News

MAHAFALI

TANGAZO LA MAHAFALI

Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wanafunzi wote waliomaliza masomo yao katika mwaka wa masomo wa 2018/2019 kuwa Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 13 Disemba 2019 katika Kampasi ya Ubungo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb). Aidha wahitimu wanaotaka kushiriki Mahafali hayo wathibishe ushiriki wao kupitia akaunti zao za SIMS na kulipia Tshs. 32,000/= (Joho 30,000 na kitabu cha mahafali 2000) kabla ya tarehe 04 Disemba 2019.

Mazoezi ya mahafali hayo yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 12 Disemba, 2019 saa nane na nusu mchana Chuoni.

Kwa mawasiliano

Mob: 0768 495 124

Email: registrar@waterinstitute.ac.tz

IMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA CHUO

WOTE MNAKARIBISHWA.

Posted on 27th November, 2019